×

Bella kuja na DVD za miaka 10, Julai 22

BELLAOVER ZE WEEKEND

KWA mara ya kwanza King of The Best Melodies, Christian Bella ‘Obama’ anatarajiwa kuja na DVD za kutimiza miaka 10 tangu aingie kwenye muziki nchini ambapo zitapatikana katika shoo yake ya kihistoria itakayofanyika Julai 22, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Royal Village, Dodoma.

Akizungumza na Over Ze Weekend mratibu wa shoo hiyo, Renatus Gregory alisema kuwa DVD hizo zitakuwa na mfululizo wa maisha yake kimuziki na kazi zake zote tangu ameanza muziki nchini.

“Mashabiki waje kwa wingi waone shoo ya live kwa kutumia vyombo kutoka kwa mkali wa masauti, Bella ambaye usiku huo atapiga nyimbo zake zote kali kuanzia Yako Wapi Mapenzi, Safari Siyo Kifo, Nashindwa, Amerudi, Nani Kama Mama na nyingine kibao,” alisema Renatus.

Usiku huo kiingilio kitakuwa shilingi 30,000 kwa VIP na kawaida shilingi 10,000.

Leave a Comment