BADO skendo zinaendelea kumwandama mume wa zamani wa Khloe Kardashian, Lamar Odom baada ya hivi karibuni kuripotiwa kunaswa na machangudoa.
Usiku wa kuamkia Ijumaa iliyopita, Odom, mcheza kikapu wa zamani NBA akiwa na genge lake, walionekana wakiingia katika moja ya klabu za usiku na kuchomoka wakiwa na wacheza utupu kadhaa wa klabu hiyo wanaotajwa kuwa machangudoa pia, kabla ya baadaye yeye kugandana na mmojawao.
Licha ya kuzunguka nao sehemu mbalimbali lakini imeelezwa kuwa safari yao iliishia nyumbani kwa Odom majira ya saa 10 alfajiri.
Wakati ikiwa hivyo, upande wa pili taarifa zinasema kuwa Odom anayeandamwa na majanga kila kukicha, amesitishiwa mkataba wake wa kwenye Shoo ya Keeping Up With The Kardashians, sehemu pekee aliyokuwa akiitegemea kuingiza pesa kwa kipindi hiki.
