The House of Favourite Newspapers

Licha ya Nay wa Mitego… TRA wamhenyesha Diamond siku 7

0

diamond Nasibu Abdul ‘Diamond’

MUSA MATEJA, Amani

DAR ES SALAAM: Imevuja! Siku chache baada ya Mbongo Fleva, Emanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ kukamatwa na kuhojiwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kuhusu chanzo cha utajiri wake wenye utata, mwenzake katika fani, Nasibu Abdul ‘Diamond’ naye amekumbana na kimbembe cha kuchunguzwa na TRA, Amani lina kitu mkononi.

TRA ni Mamlaka ya Mapato Tanzania ambayo inajishughulisha na ukusanyaji wa kodi kwa wafanyabiashara na wananchi kwa jumla ili kuiletea nchi maendeleo kutokana na pesa hizo za kodi.

dc49DIAMOND11CHANZO KINASEMA

Kwa mujibu wa chanzo, Diamond alikumbwa na kimbembe hicho Juni, mwaka huu kabla ya Nay na kwamba, jamaa wa TRA walimvamia nyumbani kwake, Madale na kutaka aorodheshe mali zake zote ili ambazo hazijalipiwa kodi zijulikane.

“Jamani, mmeandika habari za Nay kukamatwa na polisi na kuhojiwa kwa siku mbili kwa sababu ya utajiri tata. Sasa mimi nawaambia ubuyu mwingine kwamba, Diamond naye alishikwa na watu wa TRA, wakawa wanamhoji kuhusu mali zake zote.”

diamond gariWALIANZIA MADALE

“Walianzia nyumbani kwake Madale, wakaangalia uhalali wa nyumba yake na vitu vingine kama magari na vyote ambavyo vinatakiwa kulipiwa kodi.”

mama diamond tandale (1)WAKAENDA TANDALE

“Baada ya kutoka Madale, walikwenda kwenye nyumba aliyoifanyia ukarabati, ile ya Tandale (Dar). Kule nako jamaa walifanya mahesabu yao, wanajua wenyewe walichokipata.”

Diamond Studio (2)-001WAKAENDA STUDIO

“Baada ya Tandale, wakaona bado, wakaenda kwenye studio yake (Wasafi Records) iliyopo Sinza Mori, Dar, nako wakaangalia kila kitu kilichomo na uhalali wake kama havidaiwi kodi.”NYUMBA (1)

NYUMBA ALIYONUNUA

“Kama vile haitoshi, wakaenda kwenye ile nyumba aliyonunua, iliyopo Salasala, Dar ambako pia waliipigia thamani na kuangalia kama alilipia kodi kwenye manunuzi.”

ILICHUKUA SIKU SABA

“Afadhali ya Nay alihojiwa kwa siku mbili, Diamond ni siku saba, sema tu yeye, jamaa wa TRA walikuwa wanambana mchana kutwa na kumwachia jioni,” kilisema chanzo hicho.

DIAMOND ACHANGANYA AKILI

Chanzo hicho kilisema kuwa, mwisho wa kumbana, Diamond aliambiwa anatakiwa alipie kodi kwa kila kitu ambacho alikwepa kufanya hivyo.

“Lakini jamaa (Diamond), akachanganya akili zake, akaamua kumtumia kigogo mmoja serikalini ambaye alimsaidia. Kigogo huyo aliwaambia watu wa TRA wamuachie kwa sababu utaratibu waliuharibu wenyewe tangu mwanzo kwa kuacha kukusanya mapato kwa uzembe. Ndipo Diamond akaachiwa,” kilisema chanzo.

154enay2Bwa2Bmitego2BpesaNay wa Mitego.

‘KIAMA’ CHA MASTAA

Kwa mujibu wa chanzo hicho, kilichompata Diamond na Nay ni mwendelezo wa kampeni ya serikali kuhakikisha mastaa wote wanaotamba na utajiri, wanalipa kodi na pia utajiri wao uwe halali huku wale wanaomiliki utajiri usio wa halali, wakitangaziwa mwisho wao (kiama). Habari ya Nay iliandikwa Gazeti la Ijumaa Wikienda, Jumatatu iliyopita.

DIAMOND MWENYEWE

Amani lilipomtafuta Diamond ambaye kwa sasa yupo nje ya Bongo na kumuuliza kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi (meseji) kuhusu kuhenyeshwa huko, alibaki kucheka kwa kuandika ‘Teh! Teh!’ kisha akasema: “We acha tu, mambo mengine bwana!” (baada ya hapo, hakujbu tena meseji).

Juzi, Amani lilimpigia simu Mkurugenzi wa Umma wa Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo ili kumsikia anasemaje, lakini hakupokea.

Leave A Reply