The House of Favourite Newspapers

Matango, aloe vera, limao kwa kuondoa usugu kwapani

0

tango.jpegWEUSI KWAPANI

Matango ni moja ya dawa nzuri inayoweza kuondoa weusi wa ngozi ya kwapani, kama una tatizo hilo changanya na limao ili lifanye kazi vizuri, kwani nalo lina uwezo wa kung’arisha huku tango likiwa linasaidia ngozi kulainika na kuondoa ule usugu.

Bizari ya manjano

Mchanganyiko wa bizari ya manjano kidogo, juisi ya limao na juisi ya tango huweza pia kuondoka tatizo hili, kwa kupakwa kwapani na kuuacha kukaa kwa muda wa dakika tano kisha kuoshwa na maji ya baridi. Tendo hili lirudiwe mara kwa mara hadi mabadiliko ya ngozi yatakapoonekana.

WEUSI SHINGONI

Aloe vera imekuwa ikitibu magonjwa mengi na katika suala la kurekebisha ngozi ndiyo lenyewe haswa, imekuwa ikisaidia kung’arisha na kuiweka sawa.

 Jinsi ya kutumia

Paka ute wa aloe vera kwenye shingo yako hakikisha ni ile uliyoitoa shambani, bado freshi, iache kwa muda wa dakika 20 kisha osha kwa maji safi. Tendo hili nalo lifanyike mara kwa mara.

Leave A Reply