×

Esha: Mwanangu siyo haramu

ESHA (2)Stori: Hamida Hassan, Wikienda

DAR ES SALAAM: Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Esha Buheti amewacharukia wanaodai mwanaye Clarisa ni haramu, akisema kuwa wanamkosea kwani hakumzaa nje ya ndoa bali alifunga ndoa ndipo akampata.

Akizungumza na Wikienda, Esha alisema kuwa anaumizwa na watu wanaomtusi mwanaye huyo mitandaoni na kuwaomba waache na kama wanataka wamtusi yeye kwani ndiye aliyemzaa mtoto huyo.

“Unajua watu hawakuiona ndoa yangu hivyo wanadhani niliamua kuzaa tu. Hawajui kuwa nimeolewa kihalali na baada ya hapo ndiyo nikazaa hivyo wanaongea tu, naomba wasimtukane mwanangu badala yake wapambane na mimi,” alisema Esha.

Leave a Comment