×

Omog azichimba mkwara Yanga, Azam

IMG-20160623-WA0002Kocha wa Simba, Joseph Omog.

Said Ally, Dar es Salaam
KOCHA wa Simba, Joseph Omog, amesema anakiandaa kikosi chake kuja kupambana na timu yoyote ile ya ligi kuu zikiwemo Yanga na Azam huku akiahidi kuzifunga zote.
Omog, ambaye aliwahi kuinoa Azam kabla ya hivi karibuni kutua Simba, anatarajiwa kukijenga upya kikosi hicho ambacho kwa muda mrefu hakijapata mafanikio.
Kwa msimu uliopita, Simba ilionekana kuanza vizuri, lakini mwishoni ikapoteza mwelekeo na kumaliza ligi nafasi ya tatu nyuma ya Yanga na Azam.
Omog ameliambia gazeti hili kuwa, hakiandai kikosi chake kwa ajili ya kupambana na Yanga na Azam pekee, bali ni kwa ajili ya mechi zote za ligi kuu, hivyo malengo yake ni kuzifunga zote na kuwa bingwa.
“Najua Yanga na Azam ndiyo wapinzani wakubwa wa Simba, hali hiyo hainifanyi kukiandaa kikosi changu kuja kutoa ushindani kwa timu hizo tu bali nakiandaa kupambana na kila timu kwa nguvu ileile na kuzifunga zote.
“Malengo ya kwanza ni kuwa bingwa, lakini kama tukikosa ubingwa wa ligi kuu, basi Kombe la FA ni letu,” alisema Omog.

Leave a Comment