Kanye West ana vituko! Katika kile kilichowashangaza mashabiki wake hivi karibuni, jamaa huyo ameeleza kuwa anachukulia poa mkewe Kim Kardashian kupiga picha za utupu kwa kuwa ni hobi yake.
Mwanamuziki huyo ambaye pia anafanya modeling alisema kuwa, kumkataza Kim kupiga picha za sampuli hiyo ni sawa na kumzuia msanii Adele Laurie Blue kuimba wakati ndiyo kitu anachokipenda zaidi.
Akaongeza kuwa, kutokana na kupenda kamchezo hako wakati mwingine humfotoa yeye na sehemu ya mwili wa mkewe inayomvutia ni nyuma kutokana na jinsi alivyoumbika.
Kim yeye alisema kuwa anaipenda miguu ya mumewe Kanye na tumbo lake, hivyo ndiyo vipo kwenye moyo wake. Kwa kifupi kila mtu alikuwa akimsifia mwenza wake.
