×

Kala: Nataka mwanangu asumbue siku ya harusi yangu

Kala Jeremiah Global (1)Mwana Hip Hop, Kala Jeremiah amefunguka kuwa anatamani afunge ndoa wakati mtoto wake akiwa mkubwa ili siku hiyo afanye usumbufu wa hali ya juu wakati wazazi wake wakiungana.

 Kala alisema hivyo akirejea harusi ya rafiki yake Roma aliyeoa miezi ya hivi karibuni ambapo katika tukio hilo, mtoto wa Roma aliyezaa na mkewe alisumbua sana, jambo lililomvutia sana Kala.

“Nitafurahi sana nikifunga ndoa halafu mwanangu akiwa anasumbuasumbua pale harusini, mara kapita kule mara kaja kwa baba yake, itakuwa poa sana kama ilivyokuwa kwenye harusi ya mshikaji wangu Roma,” alisema Kala.

Kala kwa sasa anatamba na Wimbo wa Wana Ndoto akiwa kamshirikisha Miriam Chirwa na wimbo huo kaufanya ili kufikisha kilio cha watoto wengi wasioweza kujitetea.

Leave a Comment