×

Wenyewe wanataka niwauze – Kelvina

KELVINANa Hamida Hassan

Mwanadada anayeuza nyago kwenye filamu za Kibongo, Kelvina John ameibuka na kudai kuwa anashangaa kunyooshewa kidole kuwa anawauza mastaa wenzake wakati wenyewe ndiyo wanataka awatafutie mabwana.

Akizungumzia tuhuma kwamba sehemu kubwa ya maisha yake anategemea kuwakuwadia mastaa kwa mapedeshee, Kelvina alisema kuwa mchezo huo wanaufanya watu wengi hivyo yeye asilaumiwe kweni hata hivyo siyo kwamba anawalazimisha.

“Unajua watu wanasema eti mimi nawauza mastaa, sasa jamani kama mtu anakufuata mwenyewe na kukuambia umuunganishe kwa mwanaume f’lani mwenye nazo utakataa? Kwa kifupi wanataka wenyewe niwauze bwana…,” alisema Kelvina.

Leave a Comment