Mshambuliaji ya Yanga, chini ya Mzimbabwe, Donald Ngoma.
Nicodemus Jonas,
Dar es Salaam
KESHO Jumamosi, Yanga inatarajiwa kucheza dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Taifa kama sehemu ya kujiweka sawa kuelekea mchezo wa marudio na MO Bejaia ya Algeria kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, hata hivyo beki tegemeo wa Mtibwa, Salim Mbonde ametoa neno.
Kikosi cha timu ya Ntibwa.
Mbonde amesema kuwa safu ya ushambuliaji ya Yanga, chini ya Mzimbabwe, Donald Ngoma si lolote.
Ngoma na Amissi Tambwe pacha yao iliongoza kwa mabao msimu uliopita katika Ligi Kuu Bara ambapo jumla walifunga mabao 38 lakini Mbonde amesisitiza kuwa uwezo wa mchezaji mmojammoja, Yanga haina wachezaji wa kutisha ila wanabebwa na mfumo mzuri wa timu.
“Ngoma na Tambwe wote nimekutana nao sikuona ubora wao, sema tu wanabebwa na ubora wa timu kwa jumla. Yanga ina kikosi kizuri, wanacheza kitimu zaidi ndiyo maana yeyote anaweza kuwadhuru.
“Ila kwa ukali wa Ngoma wala Tambwe kwangu sioni wa kunishtua. Mimi naiogopa Yanga kwa jumla,” alisema beki huyo wa kati wa Taifa Stars.
Ajitabiria kipigo mapemaa
“Kuhusu mchezo wetu wa Jumamosi na Yanga licha ya kuwa ni wa kirafiki lakini utakuwa mgumu, sisi hatuna muda mrefu tangu tumeanza kuwa pamoja wenzetu hawajapumzika tangu ligi imalizike, lazima tukubali mechi itakuwa ngumu.”

