×

Video: Jamaa Atoka Singida Hadi Dar kwa Miguu na Ujumbe kwa JPM

ATOKA SINGIDA (4)Mohammed Nasoro akihojiwa na Global TV Online baada ya kuwasili Dar akitokea Singida kwa miguu.

STORI: Kelvin Shayo , Risasi Jumamosi

DAR ES SALAAM: Mkazi wa Kata ya Majengo mjini Singida, Mohammed Nasoro, amefanya tukio la kushangaza kufuatia kutoka mkoani kwake kwa baiskeli akiwa na mtoto wake, Yusuf mwenye miaka miwili na miezi 6, kwa lengo la kumpa ujumbe na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli ‘JPM’ kwa kazi nzuri anayoifanya ya kupambana na ufisadi.

ATOKA SINGIDA (3)Mtoto wake, Yusuf.

Akizungumza na Risasi Jumamosi juzi jijini Dar, Mohammed alisema safari yake ya kumuona JPM ilianza Julai 20, mwaka huu kwa kumuaga mkewe, Moza Fundisha na majirani zake ambapo kabla ya kufika Dar, alianzia Dodoma kwenye Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika Julai 23, mwaka huu.

ATOKA SINGIDA (2)Hata hivyo, katika mkutano huo, ‘mpambanaji’ huyo alisema hakufanikiwa kumwona rais jambo ambalo lilimfanya kuendelea na safari mpaka Dar alikofikia kwenye Ofisi Ndogo za CCM zilizopo Mtaa wa Lumumba ambako aliambiwa rais alikuwa ‘bize’ na ziara ya mikoani lakini akaahidiwa kwamba, akimaliza watamkaribisha kwenye hafla ya kumpongeza rais.

ATOKA SINGIDA (1)“Leo (juzi) ni siku ya pili niko hapa. Safari yangu kutoka Singida imechukua siku 12 njiani, ninamuomba Mungu anisaidie kutimiza malengo yangu kwa sababu Rais Magufuli anafanya kazi nzuri sana,” alisema Mohammed.

Mbali na hilo, Mohammed alizua gumzo baada ya kusema kuwa anamuandaa mwanaye huyo kuwa rais wa Tanzania kwa miaka ijayo.

“Ninamuandaa kijana wangu kuwa rais, kwanza kwa kumpandikizia mbegu ya ujasiri na kumpatia elimu bora itakayomsaidia kufikia kile ambacho mimi ninakiwaza kwa sasa. Nakumbuka akiwa na umri wa mwaka mmoja tu aliwahi kutamka kuwa yeye ni rais jambo linalonipa nguvu katika safari yangu ya sasa,” alisema Mohammed.

Mohammed alizungumzia pia changamoto alizokumbana nazo kwenye safari yake hiyo kwamba ni pamoja na vitisho kutoka kwa watu aliyosema ni wa vyama vya upinzani ambao wengine walifikia hatua ya kumtishia maisha.

Changamoto nyingine ni kumtunza mwanaye huyo lakini zaidi ilikuwa ni uchovu wa safari maana alikotoka ni mbali kwa usafiri wa baiskeli.

Full interview na Mohamed, Tazama hapa chini www.globaltvtz.com

Leave a Comment