×

Man Fongo: Bangi, kukaba sasa basi

MAN FONGO (3)Stori: Gabriel Ng’osha

MKALI wa Singeli anayetamba na Wimbo wa Hainaga Ushemeji, Amani Hamisi maarufu kama Man Fongo, amefunguka kuwa emevuta bangi na kukaba kwa muda mrefu, lakini sasa ameacha na kujikita kwenye muziki.

Man Fongo, alifunguka hayo kupitia Global TV Online kuwa ameishi katika maisha ya utukutu kwa kuwa hakuwa na kitu cha kufanya, ila kwa sasa muziki umembadilisha.

“Nimekaba, nimekula sana wida (bangi) lakini kwa sasa nimeacha, najitahidi kuwatengenezea mazingira pia masela wangu ili na wao waepukane na vitendo viovu, wafanye dili halali,” alisema Man Fongo.

Leave a Comment