×

Gigy Money: Sijawahi kuachana na Alikiba

GIGY (1)Gigy Money

Stori: Gladness Mallya

MWANADADA asiyeishiwa matukio Bongo, Gift Stanford ‘Gigy Money’ amefunguka kuwa hajawahi kuachana na staa wa muziki Alikiba Saleh kama watu wanavyodhani, bali bado wapo wanaendelea na mapenzi.

kibaKiba

Akipiga stori na Za Motomoto News, Gigy alisema japokuwa Alikiba yupo na Jokate Mwegelo, lakini bado ni mpenzi wake kwani walikotoka ni mbali hivyo haoni wivu wala tatizo kwenye suala hilo la ‘kushea’ mwanaume.

“Bado Alikiba ni mpenzi wangu, pale mmoja wetu anapomuhitaji mwenzake huwa tunatafutana, suala la Jokate kuwa na ujauzito wake wala haliniumizi,” alisema Gigy Money.

Leave a Comment