×
Global Publishers
  • Home
  • Habari
    • Kimataifa
    • Kitaifa
  • Global TV
  • Magazeti
  • Ajira
  • Burudani
    • Audio Music
    • Music Videos
    • Dar Live
  • Michezo
  • Makala
    • Afya
    • Mahaba & Maisha
    • Burudani
    • Hadithi
    • Mikasa
    • Siasa
  1. Home
  2. Habari
  3. Rio Olympic: Fursa kwa Vijana, Watembea Wakiuza Kondom Mitaani

Rio Olympic: Fursa kwa Vijana, Watembea Wakiuza Kondom Mitaani

Global Publishers August 13, 2016 0 Comments
SHARE THIS:

rio-staff-member-handing-out-condoms-olympic-village-081215

Rio, Brazil

WANAMICHEZO wengi walioko Rio nchini Brazil kwa ajili ya michuano ya 2016 Rio Olympics wameonekana kufanya vitu tofauti sana mwaka huu ili kuwawezesha kila mmoja kupata kile anachokidhamiria kwenye mashindano hayo. Kila mmoja yuko ‘bize’ kujituma ili ahakikishe angalau anapata medali kama ilivyo kawaida kwa tuzo za mashindano hayo.

Matukio mengi yameripotiwa kutokea huko Rio, lakini kuna hili la njemba mmoja aliyejulikana kwa jina la Eric, yeye na vijana wenzake wamekuwa wakitembea na mifuko ya kondomu mitaani huku wakihamasisha ngono salama kwa wanamichezo hao.

Wamekuwa wakionekana kwenye maeneo tofauti katika Jiji la Rio huku wakiuza kondomu hizo tena hadharani kama machinga anavyotembeza vyombo na nguo mtaani tena bila aibu. Hii imeonekana kuwa fursa kwa vijana hao kwenye mashindano kwa kuwa kuna wageni wengi ambao wanatumia zana hiyo.

Baada ya kuhojiwa na wanahabari wa E! News, Eric amejibu haya; “Mimi sioni aibu kuuza kondomu hadharani kwa maana ni biashara inayoniingizia kipato…. kuna baadhi ya wanamichezo hawafanyi kabisa ngono wakiwa kwenye mashindano makubwa kama haya, lakini kuna wengine wanaamini bila kufanya ngono hawawezi kufanya vizuri kwenye michezo yao na kupata tuzo, hao ndiyo wateja wangu haswa, ” alisema Eric.

“Kondomu pia inasaidia kujikinga na maambukizi ya virusi vya zika ambavyo kwa sasa ni tishio hapa Brazil, kwa hiyo naamini ninachokifanya siyo kosa bali nina jali afya za wanamichezo.” Alimalizia Eric.
And thus, we thank Eric and his colleagues for their service!

Meet Eric, the guy whose job it is to walk around the Olympics with a big sack of condoms pic.twitter.com/wieV9kW0N8

— Rodger Sherman (@rodger_sherman) August 7, 2016

SHARE THIS:
Previous Next

Related Posts

Balozi Wa Urusi Nchini Uturuki Auawa Kwa Risasi Akihutubia - Global Publishers FEATURED STORIES

Balozi Wa Urusi Nchini Uturuki Auawa Kwa Risasi Akihutubia

December 20, 2016
Kilombero Golf Open 2023 Yaanza leo ikiwa na udhamini kutoka NMB Bank - Global Publishers HABARI

Kilombero Golf Open 2023 Yaanza leo ikiwa na udhamini kutoka NMB Bank

October 28, 2023
Kimenuka! CHADEMA, CCM Wachapana Ngumi Dar - Global Publishers HABARI

Kimenuka! CHADEMA, CCM Wachapana Ngumi Dar

October 4, 2018
NEC Yatangaza Tarehe ya Uchaguzi Jimbo la Lissu - Global Publishers HABARI

NEC Yatangaza Tarehe ya Uchaguzi Jimbo la Lissu

July 5, 2019

Leave a Comment Cancel reply

You must be logged in to post a comment.



DAKTARI

GLOBAL TV Online




SIMBA
YANGA
NEWS
Global Publishers
  • About Us
Download on the App Store
Get it on Google Play

© 2026 Global Publishers. All Rights Reserved.

Designed by Yatosha Web Services