Na Leonard Msigwa/GPL
TUNAHAMIA Dodoma ndiyo kauli mbiu ya sasa, leo tunaangazia maeneo hatari kwa biashara ya ukahaba mjini Dodoma. Maeneo makubwa yanayotajwa kwa kukithiri kwa biashara hii haramu ni Uhindini nyuma ya benki ya NBC kwenye njia kama unaelekea Maisha Club tawi la Dodoma.
Eneo hili linavamiwa na kuwa kijiwe cha akina dada poa kuanzia saa moja usiku na akina dada hao hukaa hadi usiku mnene wakitega mawindo yao waweze kuambulia chochote.

Haya yanafanyika huku wahusika wakijua ni kinyume na maadili na sheria za nchi yetu, na kadri siku zinavyozidi kwenda biashara hii ya ukahaba inazidi kushamiri mjini Dodoma.
Maeneo mengine ambako biashara hii hufanyika kwa uwazi nyakati za usiku bila woga ni sehemu za baa kubwa hasa ile iliyopo pembezoni mwa mji na nyingine iliyopo katikati ya mji pembezoni mwa barabara ya kuelekea uwanja wa ndege wa Dodoma Mjini.
