×

Hawatakiwi na timu zao…

ISTANBUL, TURKEY - Thursday, February 26, 2015: Liverpool's Mario Balotelli before the UEFA Europa League Round of 32 2nd Leg match against Besiktas JK at the Ataturk Olympic Stadium. (Pic by David Rawcliffe/Propaganda)LONDON, England

LIGI kubwa barani Ulaya zilianza wikiendi iliyopita kwa timu mbalimbali kutinga uwanjani zikitafuta ushindi.

Kila timu ilianza kwa kuonyesha uwezo wake huku timu kadhaa zikionyesha kiwango cha hali ya juu tofauti na matarajio ya wengi.

Ligi Kuu England imeanza huku baadhi ya wachezaji wakionekana kuwa hawana nafasi hata kidogo kwenye timu zao.

Wengine wamekuwa na ugomvi na makocha huku wengine wakiwa hawatakiwi na mabosi wa timu hizo lakini wengine wakiwa hawana hamu ya kuendelea kuwa kwenye timu hizo kutokana na kutaka kwenda sehemu nyingine au wakiwa wameshuka kiwango.

Awali Juan Mata wa Manchester United alikuwa hapa kutokana na kuingizwa uwanjani na kutolewa tena na kocha Jose Mourinho kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii kutokana na wawili hawa kutokuwa na uhusiano mzuri tangu wakiwa kwenye timu ya Chelsea.

Lakini mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu England kati ya Manchester United na Bournemouth juzi ambao mchezaji huyo alianza na kufunga umemfanya atoke kwenye chati hii.

liverpool-benteke-christian-anfield_3338839Christian Benteke (Liverpool)

Liverpool msimu huu imefanikiwa kufanya usajili wa wachezaji wengi wazuri akiwemo mshambuliaji Sadio Mane aliyejiunga na timu hiyo akitokea Southampton na Georginio Wijnaldum aliyetokea Newcastle.

Kuingiza wachezaji hawa kunamaanisha kuwa sasa Benteke hana nafasi tena kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Jurgen Klopp, ambaye kuanzia msimu uliopita alimwambia kuwa anatakiwa kufanya juhudi kubwa kama anataka kucheza kwenye timu yake.

Benteke hakucheza mchezo wa kwanza wa Ligi kuu England dhidi ya Arsenal na hana nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

Sasa mshambuliaji huyo raia wa Ubelgiji anawindwa na kikosi cha Crystal Palace, na ili kipaji chake kiendelee kuwa hai ni lazima aondoke kwenye kikosi cha Liverpool.

eliaquim-mangala-3Eliaquim Mangala (Manchester City)

Huyu ni kati ya mabeki ambao walisajiliwa kwenye kikosi cha Manchester City kwa fedha nyingi na kupewa matumaini makubwa ya kutumika uwanjani, lakini mambo sasa yamekuwa magumu.

Mangala pamoja na kwamba alisajiliwa kwa kitita cha pauni milioni 42, ameshaonyeshwa hana nafasi kwenye timu hiyo ya jiji la Manchester baada ya kocha Pep Guardiola kumsajili beki wa Everton, John Stones.

Guardiola ameshamueleza mchezaji huyo kuwa anatakiwa kutafuta timu nyingine kama anataka kucheza, kocha huyo anaonekana Stones ndiye atakuwa chaguo lake namba moja kwenye kikosi cha City kwa sasa na Mangala ambaye alikuwa chaguo la kwanza la kocha Manuel Pellegrini, hawezi kupata tena nafasi ya kutumika kwenye timu hiyo.

hi-res-4719f0348503b55e3dc3d88583831fc1_crop_exactNabil Bentaleb (Tottenham Hotspur)

Alikuwa akitajwa kama mmoja kati ya wachezaji mahiri duniani, lakini kwa kocha wa Spurs wa sasa, Mauricio Pochettino, Bentaleb hana nafasi.

Staa huyo raia wa Algeria mwenye umri mdogo wa miaka 21 tu, tayari hana nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha Spurs baada ya kuzidiwa uwezo na Eric Dier na Mousa Dembele, kuanzia msimu uliopita.

Lakini pia kuwasili kwa kiungo mahiri Victor Wanyama kunaonyesha kuwa hii ni tiketi kwa mchezaji huyo kwani hawezi kupata nafasi kwenye mchezo wowote wa timu hiyo kutokana na kuwa na viungo wengi bora.

Habari zimekuwa zikisema kuwa anaweza kwenda Juventus, lakini pia ametajwa mara kwa mara kuwa anaweza kwenda kwa mkopo kwenye kikosi cha Benfica.

Bastian SchweinsteigerBastian Schweinsteiger (Manchester United)

Kocha Jose Mourinho hakuwa na kificho aliposema kuwa kiungo huyo raia wa Ujerumani hana nafasi ya asilimia kubwa kucheza kwenye timu yake msimu huu.

Schweinsteiger, pamoja na kwamba alikuwa akipata nafasi kwenye kikosi cha United chini ya kocha Louis van Gaal sasa ameelezwa kuwa ni vyema akatafuta timu ya kwenda ambayo anaweza kupata nafasi kuliko kubaki United.

Kwenye mchezo wa juzi dhidi ya Bournemouth mchezaji huyo hakupata nafasi hata ya kukaa kwenye benchi.

Samir_Nasri_Manchester_City_vs_Chelsea_at_Busch_Stadium-2Samir Nasri (Manchester City)

Kama ilivyo kwa Mangala, Jesus Navas na Wilfried Bony, hawa wote walisajiliwa na kocha Manuel Pellegrini lakini wakashindwa kuonyesha makeke yao.

Nasri akiwa na miaka mitano kwa sasa baada ya kutokea Arsenal anaonekana kuwa anatakiwa kuondoka kwenye timu hiyo.

Kiungo huyo matata, amekuwa akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara hali ambayo imekuwa ikimnyima nafasi ya kuonyesha kiwango chake.

Sasa kocha Guardiola ameshamuonyesha kuwa anatakiwa kuondoka kwenye timu hiyo akatafute changamoto sehemu nyingine, lakini pia ameambiwa afanye kwanza kazi kubwa ya kupunguza uzito.

Mchezaji huyo amekuwa akifanya mazoezi peke yake kwenye uwanja wa mazoezi wa timu hiyo.

Phil-JagielkaPhil Jagielka (Everton)

Walipoondoka mastaa Tony Hibbert na Leon Osman, kwenye timu ya Everton iliaminika kuwa ndiyo nafasi kwa jamaa huyu kucheza kikosi cha kwanza lakini sasa mambo yamebadilika na kuwa magumu zaidi kwa mkongwe huyo kuliko msimu uliopita.

Jagielka alianza kuonekana kuwa hana nafasi kwenye timu hiyo tangu kwenye michezo ya maandalizi ya msimu, baada ya Ashley Williams aliyesajiliwa hivi karibuni kupewa nafasi kubwa ya kukaa kwenye safu ya ulinzi ya Everton.

Pamoja na kwamba amepewa unahodha, lakini anaonekana kuwa anaweza kutumika zaidi akiwa kwenye benchi kutokana na kuwa na umri wa miaka 33 kwa sasa japo kwenye mechi dhidi ya Spurs aliweza kuanza.

mario-balotelliMario Balotelli (Liverpool)

Mwanzoni mwa michezo ya maandalizi ya msimu kocha wa Liverpool Jurgen Klopp alisema kuwa Mario Balotelli hana nafasi ya kwenye timu yake.

Balotelli ambaye msimu uliopita alicheza AC Milan kwa mkopo ameonekana kushuka kiwango kwa kasi kwa siku za hivi karibuni na kocha huyo wa Liverpool ameshamwambia atafute timu nyingine ya kuchezea.

Awali alitajwa kuwa anaweza kwenda Besiktas lakini baadaye wakasema kuwa hawawezi kumlipa mshahara mkubwa wa pauni 90,000 kwa wiki, sasa anawindwa na Chievo.

jhanuzajAdnan Januzaj (Manchester United)

Kinda huyu akiwa na miaka 21 tu, tayari ameshaonyeshwa kuwa hatakiwi kwenye kikosi cha Manchester United.

Awali kocha wa zamani wa Manchester United, David Moyes aliwahi kusema kuwa huyu ni Johan Cruyff mpya kutokana na uwezo wake uwanjani.

Lakini ghafla mchezaji huyo raia wa Ubelgiji amekuwa akishuka kiwango na sasa hana nafasi kwenye timu ya United akiwa amepelekwa kwa mkopo Sunderland.

Hatari; Bi Harusi Aliyetekwa Siku ya Send Off Yake

Basata; Nay wa Mitego Huru Kuendelea na Muziki

Wema na Mama Yake Hii ni Zaidi ya Movi……

Masanja Mkandamizaji Avunja Mbavu Watu Kwenye Harusi Yake

Harusi ya Masanja Ilivyotikisa Jijij la Dar es Salaam………

Harusi ya Masanja Mkandamiza Ilivyoacha Stori Midomoni mwa Watu….

Leave a Comment