Rapa maarufu wa Marekani Young Thug yuko mbioni kuachia albamu yake mpya yenye nyyimbo 7 aliyoipa jina la Jeffery
Akizungumza wakati wa mahojiano ya moja kwa moja na Travis Scott’s.wav radio show Ijumaa (Aug. 19), Thugger aliyekuwa amevalia jinsi ya bei mbaya ya kiasi cha dola $80,000 sawa na Tsh. milioni 174.4 alisema kuwa albamu yake hiyo itakuwa na nyimbo zenye maudhui kama alizokuwa akiimba mkali wa Pop, Marehemu Michael Jackson.
“Hii ni siri,” alisema Thug. “Nachokiamini mwisho wa siku, kila mtu ataipenda albamu hii, ‘Your name Jeffery.’ Hakuna wimbo wowote wenye maudhui kama mlivyonizoea (Thug) kwenye nyimbo zangu zilizopita. Kuna ‘Cool music’ kama Pop za Michael. Kuna wimbo mmoja nimeufanya humo unaitwa ‘Future Swag’ lakini una maudhui mapya ya Jeffery.”
Thug alisema ameamua kubadilika na kurudi kwenye asili yake ya uimbaji mbapo atakuwa anaimba Melody kama za Michal Jackson kwani ndiko alikoanzia kabla ya kuanza ku-rap.
“Sikuwahi kufikiria kama ipo siku nitakuja kuwa rapa, kwa kuwa sikuwa na mawazo ya kimtaa zaidi, nilikuwa naimba kama Michael Jackson alivyokuwa akiimba” Thug alisema. “Sasa narudi vile nilivyokuwa mwanzo, nakuwa Jeffery halisi. Hii ndiyo swag zangu.”
Thug ambaye anataka kubadili jina lake na kuitwa No, My Name is Jeffery aliongeza kuwa hajawahi kuuza ngada (madawa ya kulevya) kama anavyoandamwa kwenye mitandao ya kijamii na anataka kuachana na bifu anazoziita za kijinga dhidi yake na Lil Wayne pamoja na The Game ili aishi maisha yasiyokuwa na chuki na mtu yeyote. Thug anatarjia kuachia mixtape ya albamu yake mpya kabla ya mwezi Septemba mwaka huu.

nampenda sana rapa young thug, namtakia Safari njema na mafanikio mema, but tamkumbuka Sana Kwani. nimekuwa nikimfuatilia long time. my name is Kon thug from Tanzania.