Gari likiwa limepinduka.
MTU mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja amenusurika kifo baada ya gari alilokuwa akiliendesha kuacha njia na kupinduka.
Wasamaria wema wakiangalia jinsi ya kumtoa jamaa huyo.
Tukio hilo ambalo lilijaza watu kibao limetokea maeneo ya Tabata-Barakuda ambapo jamaa huyo akiwa anakatisha njia ya vumbi inayoelekea Yombo akiwa kwenye mwendo wa kasi aliparamia kifusi cha kokoto kilichokuwa pembeni mwa barabara na kusababisha gari lake kupinduka.
Watu walijaa eneo la tukio ambapo walifanikiwa kumuokoa jamaa huyo akiwa hana jeraha lolote huku wakiendelea na jitihada za kuligeuza gari hilo ambalo lilionekana kuharibika vibaya.
Jamaa (mwenye shati la bluu) baada ya kutolewa kwenye gari akiwa hajaamini macho yake.
Stori/Picha: Gladness Mallya/GPL

