The House of Favourite Newspapers

Tetemeko la Ardhi Laua 6 Italia

0

UmbriaWATU takribani sita wanahofiwa kupoteza maisha kutokana na tetemeko kubwa la ardhi lililoukumba Mji wa Umbria uliopo katikati mwa Italia huku makazi mengi ya watu yakiharibiwa vibaya na tetemeko hilo.

Tetemeko hilo lilianza kutokea mara baada ya kuangusha nyumba moja na kuuwa watu wawili wanaodaiwa kuwa ni wanandoa katika eneo la Pescara del Tronto mkoani Marche na kuanza kusambaa kuelekea Mashariki huku likiharibu vibaya makazi ya watu na kusababisha maafa makubwa.

UmbriabBaadaye raia mwingine aliripotiwa kufariki dunia na wanafamilia wanne wakiwemo watoto wawili baada ya nyumba yao kuangushwa na tetemeko hilo huko Accumoli. Meya wa mji huo alisema.

Watafiti wa Marekani wamesema kitovu cha tetemeko hilo kilikuwa katika mji wa Norcia, karibu na Perugia ambapo nguvu ya tetemeko hilo linakadiriwa kuwa ni ritcha 6.2 na lilikuwa mbali kidogo na Mji wa Roma na Venice.

UmbriacWaziri mkuu wa Italia, Matteo Renzi, amesema serikali yake inaendelea kuwasiliana na taasisi za kiraia la ulinzi wa nchi hiyo. Maeneo ambayo yameripotiwa kuathirika zaidi ni Amatrice, Accumoli, Posta na Arquata del Tronto

Leave A Reply