Este Kiama: Mtoto wangu ndiye faraja yangu
Ester Kiama akipata kifungua kinywa nyumbani kwake..
Mambo vipi mpenzi msomaji wa safu hii maridhawa ya Mpaka Home. Wiki hii nilitia nanga maeneo ya Kijitonyama, jijini Dar nyumbani alikopanga msanii wa filamu mwenye mvuto ambaye amedhamiria kuleta mapinduzi kwenye sanaa, Ester Kiama.
Staa huyu anishi na mtoto wa kiume aitwaye Brian (5) pamoja na wadogo zake, twende pamoja chini:
Ester Kiama na mjwanaye.
ANA MAISHA YA AINA GANI?
“Maisha yangu ni ya kawaida sana wala sipendelei kuyakuza wala kuyabadilisha tofauti na nilivyokuwa nikishi huko nyuma.”
ANAZUNGUMZIAJE MAISHA YA UMAARUFU?
“Tofauti ni kubwa sana, zamani niliweza kutembea zangu na kula hata muhogo njiani lakini sasa nakuwa siwezi maana kila mtu anakutazama unachofanya.”
RATIBA YAKE YA SIKU NZIMA IPOJE?
“Mara nyingi napenda kuamka mapema kwa ajili ya kumuandaa mwanangu na kufanya usafi wa nyumba, naweza kufungua kinywa au nikanywa maji ya moto kisha naendelea na ratiba yangu kama niko free naingia jikoni kupika na kama sina sehemu ya kwenda napumzika.”
ANAPENDA NYUMBA YAKE IWEJE?
“Kuna vitu natamani sana viwepo nyumbani kwangu kwanza kabisa napenda kuwe na boksi la kufugia samaki na bustani ya maua.”
ANAFANYA KAZI ZA NYUMBANI AU ANAFANYIWA NA HAUSIGELI?
“Muda mwingi napenda kufanya kazi zangu mwenyewe dada anaweza kusaidia vitu vingine vidogovidogo tu na kumuangalia mtoto.”
ANAISHI NA BABA MTOTO WAKE?
“Hapana naishi peke yangu maana huyo tuliachana, muda mrefu niko peke yangu na huwezi amini mtoto wangu ndiye faraja yangu.”
ANAPENDELEA MAVAZI GABNI AKIWA NYUMBANI?
“Mara nyingi napendelea mavazi ambayo yatanifanya niwe huru kama nguo fupi ama ‘skintight’ na wakati mwingine napendelea kujifunga khanga ndiyo mavazi ninayoyapenda nikiwa nyumbani.”
BAA YAKE YA NYUMBANI IMEJAA VINYWAJI NI MLEVI?
“Hapana hiyo ni moja tu ya mapambo ya nyumba yangu na ni muhimu sana kwa wageni wangu japokuwa huwa natumia kidogo siku moja moja”
ANA MATARAJIO GANI?
“Natarajia niwe na eneo langu mwenyewe nitengeneze sehemu ya kuchezea watoto, nipande maua na miti mingi na niishi sehemu iliyotulia, naamini nitayakamilisha.”