MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Enock Rashid ‘Enock Bella’, amefunguka kuwa anajitahidi kufuata nyayo za msanii ambaye anafanya vizuri kwa sasa Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz au Mondi’.
Akizungumza na Risasi Vibes, Enock amesema kuwa katika kazi zake za muziki, anajitahidi sana kufuata maajabu ambayo Diamond anayafanya kuutangaza muziki Kimataifa zaidi.
“Diamond ni msanii ambaye ni mfano wa kuigwa hapa nchini, kwa sababu amefanya jitihada nyingi kuufikisha muziki mbali zaidi na hata wasanii wengi wametambulika kupitia yeye. Hivyo mara nyingi ninapofanya kazi zangu, namuangalia sana yeye ili nifike mbali,’’ alisema Enock Bella.
STORI: Happyness Masunga, Risasi
