Mwenyekiti wa Chama cha Waendesha Bodaboda Wilaya ya Kinondoni, Almano Mdede (katikati) akisoma taarifa yake kwa wanahabari (hawapo pichani).
WAKATI Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, akitoa tamko lake la kuahirisha maandamano yaliyokuwa yamepangwa kufanyika nchi nzima chini ya wito wa Ukuta kesho Septemba Mosi, viongozi wa vyama vya waendesha Bodaboda Mkoa wa Dar es Salaam, vimeungana naye kwa kusema kuwa kama maandamano hayo yangelifanyika wao wasingeshiriki.
Katibu wa Chama cha Waendesha Bodabaoda, Oscar Wiluye (katikati) akisisitiza jambo.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chama cha Waendesha Bodaboda, Almano Leonard, alisema kuwa ilikuwa marufuku kwa wanachama wao kujihusisha na masuala mazima ya kisiasa yakiwemo maandamano hususan siku iliyokuwa imepangwa ya kesho.
…Akiendelea kuongea na wanahabari. Nyuma yake ni baadhi ya viongozi kutoka wilaya za Kinondoni, Ilala na Temeke.
Alisema kuwa isingewezekana mwanachama yeyote kubeba abiria aliyevalia sare ya chama chochote kwani hatua kali kwa ambaye angelithubutu zingelichukuliwa na viongozi wao wa wilaya.
Wanahabari wakichukua tukio hilo.
Mbowe ameahirisha maandamano hayo kwa muda wa mwezi mmoja ili kutoa fursa kwa viongozi wa dini kutafuta muafaka wa majadiliano na serikali.
NA DENIS MTIMA/GPL