×

Mr. Championi anadi muonekano mpya wa Ijumaa Kisemvule

1.Wasoamaji wakiWasoamaji mbalimbali wa eneo la Kisemvule Mkuranga Mkoa wa Pwani wakizingira gari la matangazo kwa ajili ya kununua gazeti la Ijumaa na Championi.

2.Jackline Juma (katikati) akielekezwa jambo na Ofisa masoko wa Global,Yohana Mkanda (kulia).Jackline Juma (katikati) akielekezwa jambo na Ofisa masoko wa Global,Yohana Mkanda (kulia).

3.Wasomaji wakinunua gazeti kwa muuzaji (aliyevaa fulana nyeupe) katika eneo la Kisemvule.

4.Mdau wa Gazeti la Ijumaa, Abdu Lugome (katikati) akifafanuliwa jambo na Mkanda juu ya ubora wa gazeti hilo la Ijumaa.

5.Mr.Championi akijinadi katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Mkuranga. Mbele anayeuza magazeti ni Mwamvita Rashid.

6Said Bakar akilisoma gazeti la Champion baada ya kununua kwa Mwamvita.

Mr.Championi kwa mara nyingine tena ameingia mtaani leo na kulinadi Gazeti la Ijumaa lenye muonekano mpya na gazeti la michezo la Championi kwa wasomaji mbalimbali wa Kisemvule, Dundani na maeneo mengine ya Wilaya ya Mkuranga, Pwani.

7Wasomaji wakiendelea kuchangamkia kununua gazeti.

Baada ya kutua eneo hilo la Kisemvule, Mr.Championi kazi yake kubwa ilikuwa kuyanadi magazeti hayo mawili ya Championi na Ijumaa ambapo wasomaji mbalimbali walijitokeza kwa wingi kwenye gari la matangazo la magazeti hayo na kuchangamkia kuyanunua huku pia Mr.Championi akiwapa wasomaji zawadi mbalimbali alizokuwa nazo.

8.Msomaji akipozi na Mr. Championi eneo la Mwanambaya.

Akizungumza na wakazi eneo hilo, Ofisa Masoko wa Kampuni ya Global Publishers, Yohana Mkanda aliwaomba wasomaji kuendelea kulinunua Ijumaa kwa bei ya Sh.1,000 kwani limesheheni habari nyingi za burudani, hadithi, machombezo na mikasa pia kukata kiu yao kwa kusoma Gazeti bora la Michezo Tanzania la Championi.

9.Msomaji wa gazeti la Ijumaa aitwaye, Juliana Yusto (katikati) akifafanuliwa jambo na Mkanda.

“Magazeti yote ya Global yanauzwa shilingi 500 isipokuwa Ijumaa pekee lenye muonekano mpya ndilo linauzwa shilingi 1,000. Niwasihi wasomaji wetu waendelee kununua magazeti yetu ili wazidi kuhabarika, kuelimika na kuburudika,” alisema Mkanda.

Na Denis Mtima/Gpl

Leave a Comment