×

Mamia Wachangamkia Chemsha Bongo Ya Kwenda Dubai

SAMSUNG CAMERA PICTURESDereva wa Bodaboda wa Kijiwe cha Maji Chumvi, Tabata Kisukuru, Julius akisoma Gazeti la Amani kwa umakini.

SAMSUNG CAMERA PICTURES

Wasomaji wa Gazeti la Amani, Nicodemus Salvatory (mwenye kofia) akiwa na mwenzake, Dunia Ally wakisoma gazeti hilo katika eneo la Bosnia, Tabata.

SAMSUNG CAMERA PICTURES
Msomaji wa Gazeti la Amani, Ladislaus Massawe akisoma gazeti hilo katika eneo la Kwa Urasa, Tabata.

 

SAMSUNG CAMERA PICTURESZulkifir Mputo akinunua Gazeti la Amani kutoka kwa muuzaji, Mwamvita Rashid katika eneo la Migombani, Tabata.

SAMSUNG CAMERA PICTURES
Daines Masomi akisoma Gazeti la Amani katika eneo la Koko Mtama, Segerea.

MAMIA ya wasomaji wa magazeti wameendelea kuchangamkia fursa ya Shindano la Chemsha Bongo ya kwenda Dubai inayoendeshwa katika gazeti makini la Amani linalochapishwa na Kampuni ya Global Publishers.

Timu nzima ya masoko leo ilitua katika maeneo ya Tabata, Ubungo na Segerea na kushuhudia wasomaji wengi wakilichangamkia Gazeti la Amani linalotoka kila Alhamisi.

Akizungumza na mtandao huu, Ofisa Masoko wa Global, Yohana Mkanda aliwaomba wasomaji wote wa Magazeti Pendwa hususan Gazeti la Amani lenye Chemsha Bongo ndani yake kusoma kwa wingi ili kujishindia zawadi zilizomo.

“Kwa wale wasomaji wa Gazeti la Amani hii ni fursa yao kulinunua na kushiriki chemsha bongo inayopatikana ukurasa wa pili. Mshindi anaweza kujishindia kiasi cha Sh. 500,000 hadi safari ya kwenda kuponda raha Dubai kwenye hoteli ya kifahari kwa siku tatu,” alisema Mkanda.

 

Leave a Comment