Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya simu za mkononi ya Zantel, Benoit Janin kulia), akikabidhi mbuzi 12 kwa Kaimu Mufti, Sheikh Ally Ngeruko kwa niaba ya vituo mbalimbali vya kulelea watoto yatima jijini Dar es Salaam kusherehekea sikukuu ya idd el Adha. Makabidhiano yalifanyika katika ofisi za BAKWATA, Kinondoni, Dar es Salaam jana. Wanaoshuhudia ni watoto kutoka katika vituo hivyo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya simu za mkononi ya Zantel, Benoit Janin (wa pili kulia), akikabidhi mbuzi 12 kwa vituo mbalimbali vya kulelea watoto yatima jijini Dar es Salaam kwa uratibu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) ambapo Kaimu Mufti, Sheikh Ally Ngeruko (wa pili kushoto nyuma ya watoto), alipokea msaada huo kwa niaba ya vituo hivyo. Makabidhiano yalifanyika katika ofisi za BAKWATA, Kinondoni, Dar es Salaam jana. Kulia ni Meneja Biashara wateja wa Makampuni wa Zantel, Kasongo Faraji.
Meneja Habari na Uhusiano wa Kampuni ya simu ya Zantel, Winnes Lyaro (kulia) akigawa juisi kwa baadhi ya watoto yatima katika hafla hiyo.
Meneja Biashara wateja wa Makampuni wa Zantel, Kasongo Faraji (kulia), akizungumza katika hafla hiyo ambayo Zantel ilikabidhi msaada wa mbuzi 12 kwa Kaimu Mufti, Sheikh Ally Ngeruko kwa niaba ya vituo mbalimbali vya kulelea watoto yatima jijini Dar es Salaam kusherehekea sikukuu ya Idd el Adha.

Baadhi ya wawakilishi wa vituo vya kulelea watoto yatima wakichukua mbuzi waliotolewa na Zantel.



