×

Guardiola amzima Mourinho Old Trafford

TIMU ya Manchester City leo imeshinda mabao 2 – 1 dhidi ya Manchester United  katika mchezo mkali uliopigwa Uwanja wa Old Trafford. Mabao yote yalifungwa kipindi cha kwanza, wafungaji kwa upande wa Man City ni De Bruyne aliyetupia dakika ya 15 kisha Iheanacho akaongeza la pili dakika ya 36, bao pekee la wenyeji Man United liliwekwa kimiani na Zlatan Ibrahimovic dakika ya 42.

MANCHESTER UNITED: De Gea, Valencia, Bailly, Blind, Shaw, Pogba, Fellaini, Mkhitaryan (Herrera), Rooney, Lingard (Rashford), Ibrahimovic
Subs: Mata, Martial, Smalling, Romero, Schneiderlin
Booked: Bailly, Fellaini, Ibrahimovic
Scorer: Ibrahimovic
MANCHESTER CITY: Bravo, Sagna, Stones, Otamendi, Kolarov, De Bruyne (Zabaleta), Fernandinho, Silva, Sterling (Sane), Iheanacho (Fernando), Nolito
Subs: Caballero, Jesus Navas, Clichy, Garcia
Booked: Silva
Scorers: De Bruyne, Iheanacho

38287b0b00000578-3782950-image-a-30_1473508719070

Kevin De Bruyne (kulia) akishangilia baada ya kufunga bao la kuongoza dhidi ya Manchester Utd leo katika Uwanja wa Old Trafford.

382877a800000578-3782950-image-a-32_1473508770601

De Bruyne akipiga shuti ambalo ndilo lilizaa bao la kwanza kwa Man City, huku kipa  wa Manchester United, David de Gea (kulia) akijitahidi kutaka kuokoa lakini alishindwa.

38288c7a00000578-3782950-image-a-81_1473511941799

Mourinho (kushoto) na  Guardiola wakifuatilia mechi hiyo.

3828794f00000578-3782950-image-m-39_1473508914295

Wachezaji wa Man City wakishangilia.

3828a30500000578-3782950-image-a-62_1473510433980

Ibrahimovic akishangilia baada ya kuifungia Man Utd bao.

3828ee0100000578-3782950-image-a-109_1473514269418

Kocha wa Man Utd, Mourinho akitoa maelezo kwa wachezaji wake (hawapo pichani) baada ya mchezaji wake kufanyiwa faulo.

Leave a Comment