Bwana Meddy Mulisa wa Kagondo Mweruka Kata Muhutwe anasikitika kuwatangazia kifo cha mke wake mpendwa Feliciana Mulisa kilichotokea usiku wa kuamkia jana katika Hospitali ya Mount Meru Arusha. Alifariki Sept 13.
Habari ziwafikie Askofu Desiderius Rwoma, Askofu Msaidizi Methodius Kilaini wa Jimbo Katoliki la Bukoba, Mhe Salim Kijuu mkuu wa mkoa wa Kagera, mheshimiwa Balozi Sued Kagasheki, Waandishi wa Habari, Ndugu, Jamaa na Marafiki popote walipo.
Mazishi yatafanyika Jumamosi Septemba 17 saa nane alasiri kijijini kwake Kagondo Mweruka. Apumzike kwa Amani.
