×

Wasomaji Ijumaa Muonekano Mpya Waduwazwa Na Mr. Championi

SAMSUNG CAMERA PICTURESMsomaji wa Gazeti la Championi akiwa na Mr. Championi.

SAMSUNG CAMERA PICTURESMr. Championi akipozi na wasomaji wa Gazeti la Ijumaa lenye muonekano mpya.

SAMSUNG CAMERA PICTURESMr. Championi akiwa na wasomaji wa Gazeti la Ijumaa na Championi.

SAMSUNG CAMERA PICTURESMama Lishe, Ester Mkazi wa Kimara jijini Dar akilisoma gazeti la Ijumaa. Pembeni yake ni Mr. Championi anayelinadi gazeti hilo.

SAMSUNG CAMERA PICTURESSelemani Hamis Mkazi wa Mbezi ya Kimara akilisoma Gazeti la Championi.

SAMSUNG CAMERA PICTURESMr. Championi akiwa na msomaji wa Gazeti la Ijumaa na Championi.

SAMSUNG CAMERA PICTURESMr. Championi akiwa na wasomaji wa Gazeti la Ijumaa na Championi.

WASOMAJI mbalimbali wa Gazeti la Ijumaa lenye Muonekano Mpya, leo wameonekana kuduwazwa na Mr. Championi wakati alipotua eneo la Mbezi ya Kimara jijini Dar kwa ajili ya kulinadi gazeti hilo ambapo wengi wa wasomaji walionekana  kuonesha furaha yao pale waliponunua gazeti hilo na kupiga naye picha.

Baada ya kutua maeneo hayo Mr. Championi kazi yake kubwa ilikuwa kuyanadi magazeti hayo mawili ya Championi na Ijumaa ambapo wasomaji mbalimbali walijitokeza kwa wingi kuyanunua huku pia Mr. Championi akiwapa wasomaji zawadi mbalimbali alizokuwa nazo.

Akizungumza na wakazi eneo la Kimara mwisho, Ofisa Masoko wa Kampuni ya Global Publishers, Yohana Mkanda, aliwaomba wasomaji wa magazeti hayo ya Global kuendela kulinunua Ijumaa kwa bei ya Sh.1000 kwani limesheheni habari nyingi za burudani, hadithi, machombezo na mikasa pia kukata kiu yao kwa kusoma Gazeti bora la Michezo Tanzania la Championi.

“Magazeti yote ya Global yanauzwa kwa shilingi 500 isipokuwa Ijumaa pekee lenye muonekano mpya ndilo linauzwa shilingi 1000. Niwasihi wasomaji wetu waendelee kununua magazeti yetu ili wazidi kuhabarika, kuelimika na kuburudika,” alisema Mkanda.