
…Ni majaji hao wakiwasikiliza kwa makini wanamitindo (hawapo pichani) wakijibu maswali.
Baadhi ya wanamitindo wakijibu maswali.
Wanamitindo wakiwa katika picha ya pamoja na majaji.
Wanamitindo kutoka kampuni ya mitindo ya Black Fox ya Msasani jijini Dar, jana walikuwa katika mazoezi ya mwisho kujiandaa na maonesho ya mavazi yanayotarajiwa kufanyika Oktoba 8, katika Ukumbi wa Zanzibar Grand Palace, visiwani Unguja, kwa ajili ya uchangishaji wa kusaidia wagonjwa wa saratani ya matiti waliyoyapa jina ya Marashi ya Pwani.
Wanamitindo hao jana walikuwa katika mchuoano wa mwisho ili kuwapata wanaoweza kuwa mabalozi wenye uelewa stahiki wa ugonjwa huo watakaowaeleza watu jinsi ya kujikinga na ugonjwa huo na kukabiliana nao pindi mtu anapoupata.
Majaji watakaoendesha shughuli siku ya hafla hiyo hiyo ambao ni Kulwa Nkwandule (wa kwanza kulia) ambaye ni mmoja wa waandaji , Nadia Azmat (katikati) ambaye ni mdhamini mkuu na wa mwisho ni Aj Myner.
Na Imelda Mtema.