WAJUMBE wa Baraza la Ardhi wa Wilaya ya Kinondoni wametakiwa kutobweteka badala yake waende kwa wananchi ili kujua changamoto za ardhi katika wilaya hiyo.
Mwito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Sophia Mjema Dar es Salaam juzi alipokuwa akizungumza na wajumbe hao ofisini kwake.
“Ninyi ni watu muhimu sana katika kuibua changamoto za ardhi katika kata zetu zote za wilaya ya Kinondoni nawaomba msiwe watu wa kukaa nendeni kwa wananchi huko kuna changamoto nyingi za ardhi” alisema Mjema.
Mjema aliwataka wajumbe hao kwenda kutoa elimu kwa wananchi ili wajue haki zao kuhusu masuala ya ardhi jambo litakalosaidia kupunguza migogoro ya ardhi.
Aliongeza kuwa migogoro mingi ya ardhi iliyopo katika wilaya hiyo mingi inasabaishwa na wananchi kutojua masuala ya ardhi na elimu.
CREDIT: DOTTO MWAIBALE.