Daudi Michael ‘Duma’ akiwa kajilaza chumbani kwake.
…Akiwa sebuleni.
LEO hii kwenye kolamu yetu ya Mpaka Home tunaye msanii wa filamu Bongo, Daudi Michael ‘Duma’ anayetamba na Filamu ya Mchongo Siyo, aliyewahi kujizolea umaarufu mkubwa kutokana na igizo la Siri ya Mtungi, anayeishi maeneo ya Mwananyamala A jijini Dar.
Tumezungumza naye kuhusu mambo mbalimbali ya nyumbani kwake na fani yake kwa ujumla, hapa chini anajieleza kama ifuatavyo:
Maisha yake halisi
“Mimi maisha yangu namshukuru Mungu siko vibaya kiivyo kutokana na kujituma kwenye shughuli zangu za uigizaji, nimeweza kupanga hii nyumba, isitoshe katika maisha ya kawaida ni mtu poa najichanganya sana, ndiyo maana hata bethidei yangu juzikati nilifanya kitaani kwetu tu, lakini wasionijua wanasema naringa.
Anaishi na nani?
“Humu ndani naishi mwenyewe, najifanyia kila kitu. Nina watoto wawili; wa kwanza Mariamu (3) wa pili Brashal ana miezi minne kila mtu na mama yake, wote nimeachana nao tulipanga kuzaa tu.
Kuhusu kuoa
“Kifupi naishi kisela japo nina mtu wangu ambaye tunapendana na tunaheshimiana, sijafikiria suala la ndoa kwa sasa bado kuna mambo nayaweka kwenye mstari.
Daudi Michael ‘Duma’ akiwa kajilaza chumbani kwake.
Kuhusu kusumbuliwa
“Kiukweli usumbufu ni mkubwa mno hususan mitandaoni, lakini mimi si mtu wa shobo kwa mademu sababu kila kizuri ukitaka uwe nacho mwisho wake ni mbaya lazima utaangamia na mimi bado kijana yaani damu changa kabisa, lazima niwe makini kuilinda afya yangu nisije kufa kabla ya wakati maana Ukimwi si ugonjwa wa mchezo.
Siri ya muonekano wake!
“Najitambua kwamba nina muonekano mzuri ambao ni kivutio kwa wadada wengi wa mjini, lakini siri kubwa ni mazoezi, kila siku nikiamka huwa nazingatia mazoezi kuliko chochote, ndiyo maana wengi wamekuwa wakiniuliza hilo swali na kutaka niwape mbinu ya mafanikio, tatizo vijana wengi sio watu wa tizi. Kupumzisha mwili, vyakula na si mtu wa starehe.
…Akipanga kofia chumbani kwake.
Kuhusu ufuska Bongo MUVI…
“Siku zote wanasema samaki mmoja akioza ni wote, lakini si kweli lazima wanakuwepo waliosalia, hayo mambo yapo lakini kwa baadhi maana kwenye tasnia tunakutana watu wa kila namna na kila rika, ni vigumu kubadili tabia ya mtu ikiwa hujapaswa kuibadili, ukitaka hilo ni lazima uache kazi ufanye kazi.
Wasanii kutopenda kuoa mastaa…
“Haina ubishi kwamba ndoa za mastaa kwa mastaa ni chache mno, kwa sababu tunakuwa tunajuana tabia kiundani haswa kwamba wengi hawajatulia, hata kama ikitokea wasanii kwa wasanii mkiwa wapenzi lakini malengo hakuna mnadanganyana tu, si unajua watu wana watu wao wengine tangu zamani?”

