The House of Favourite Newspapers

Mourinho ashtakiwa na FA kwa kumuingilia refa

Mourinho-Lampard-City-513573KOCHA Mkuu wa Manchester United, Jose Mourinho ameshtakiwa na Shirikisho la Soka Nchini Uingereza, FA kwa kudai kwamba itakuwa vigumu kwa refa Anthony Taylor kusimamia mechi yao dhidi ya Liverpool.

Mourinho aliongezea kwamba, kumteua Taylor kusimamia mechi hiyo ya tarehe 16 Oktoba ilimpatia shinikizo refa huyo mwenye makao yake Manchester.

Mameneja hawaruhusiwi kuzungumzia kuhusu marefa kabla ya mechi.

Mourinho amepewa muda hadi Oktoba 31 awe amejibu shtaka la ukosefu wa nidhamu na kusababisha mechi hiyo kuwa na jina baya.

Taylor alitoa kadi 4 za njano zote kwa timu ya Manchester United katika sare hiyo ya 0-0.

Comments are closed.