×

Shigongo: Uongozi Bora Huanzia Ngazi za Chini

eric-shigongo-1

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers, Eric Shigongo, akifundisha katika semina hiyo.

eric-shigongo-2

…Akiendelea kuelezea masuala mbalimbali.

eric-shigongo-3

Baadhi ya wanasemina wakifuatilia kilichokuwa kikiendelea.

eric-shigongo-4

Shigongo na mkewe Veneranda Kavishe (kulia kwake) wakifuatilia hotuba zilizokuwa zikitolewa na wazungumzaji wengine.

eric-shigongo-5

Mkurugenzi wa The Global Leadership  Summit,  Mbutho Chibway, akizungumza katika semina hiyo.

eric-shigongo-6

Shigongo akielezea historia ya Severin (aliyesimama mbele ya wanasemina) baada ya kumaliza kifungo chake gerezani.

eric-shigongo-7

Baadhi ya wanasemina wakifuatilia hotuba za viongozi mbalimbali wa kimataifa kwenye TV .

eric-shigongo-8

Baadhi ya wanasemina wakimfariji Severini (katikati) baada ya kumalizika semina hiyo.

eric-shigongo-9

Shigongo akihojiwa na wanahabari.

eric-shigongo-10

Mahojiano na wanahabari yakiendelea.

MKURUGENZI Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers, Eric Shigongo,  amesema uongozi bora popote unatakiwa kuanzia katika ngazi ya chini kwanza kwani huko ndiko kwenye mizizi.

Hayo ameyasema jana kwenye ukumbi wa mikutano wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam alipokuwa akifundisha katika semina iliyojulikana kwa jina la The Global Leadership  Summit juu ya mbinu mbalimbali za kuwa kiongozi bora wa kitaifa na kimataifa.

Akizungumza katika semina hiyo Shigongo alisema  uongozi ni dhamira kutoka moyoni mwa mtu husika kwa kushirikiana na watu wanaomzunguka.
Alisema uongozi ni karama ya mtu kutoka moyoni mwake, akatolea mfano wa mtu anayefanya kazi ya usafi ofisini anavyoweza kuwa mbunifu zaidi na kuzidi watu wengine.

Alisema viongozi wa Kiafrika wanashindwa kuendelea kwa sababu ya uongozi mbaya na akasema Afrika inapaswa kubadilisha mfumo wa  maisha ili iweze kuwa na uongozi bora.
Aliwaomba wanasemina hiyo kutumia fursa hiyo kutoka kwa wazungumzaji mbalimbali kuhakikisha wanawekeza kwenye uongozi thabiti.

Miongoni mwa mambo aliyofundisha ni kuwa na lengo, ubunifu, kuwa na mtazamo wa mbele na kujifunza kutoka kwa watu wengine.
Wanasemina walipata fursa ya kujifunza mambo mengi kupitia televisheni iliyokuwa ukutani ikiwa na hotuba za viongozi mbalimbali wa kimataifa na kimataifa.

Shigongo aliwataka kutokata tamaa kutokana na mambo wanayokumbana nayo huku akimtolea mfano mtu mmoja aliyemtaja kwa jina la Severin aliyefika ofisini kwake Global Publishers (siku tatu nyuma) baada ya wiki kadhaa yeye kutoka katika Gereza la Ukonga kwenye tamasha alipowafundisha wafungwa  mbinu mbalimbali na kuwatia moyo.

Alimwelezea mtu huyo historia yake baada ya kumaliza kifungo chake cha zaidi ya miaka 20 jela alipoingia akiwa mdogo na hivi sasa ni mtu mzima na anahitaji kupatiwa msaada wa mawazo na hata wa kiuchumi.
Semina hiyo ya siku mbili iliyoandaliwa na The Global Leadership  Summit chini ya Mkurugenzi wake,  Mbutho Chibwaye, ilimalizika jana.

Na Denis Mtima/GPL