
Na GABRIEL NG`OSHA| GAZETI LA AMANI| SHOW BIZ-XTRA
MKONGWE wa Bongo Fleva, Seif Shaban ‘Matonya’ au ‘Shilingi ya Nyerere’ amesema kuwa kumbebesha mwanamke mimba siyo jambo jepesi kwani ni ishu inayohitaji maridhiano.
Matonya alifunguka ishu hiyo baada ya kuulizwa na Show Biz Xtra kama alishawahi kubambikiwa mimba katika maisha yake.

“Miaka kadhaa nyuma iliwahi kunitokea, sikuwa nimejiandaa ‘so’ nilijilaumu sana kwa kutokutumia kinga, maana suala la mtoto linahitaji maridhiano ya pande zote. Mkikurupuka mnazaa halafu mtoto anakuja kuteseka,’’ alisema Matonya.