×

Dk Kingwangala Aongoza Matembezi Kusaidia Ocean Road

dk-kigwangalla-1

Naibu Waziri  wa Afya, Maendeleo ya Jamii,  Jinsia,  Wazee na Watoto  Dk. Hamisi Kigwangalla akiwahutubia wananchi waliojitokeza kwenye zoezi hilo la kukusanya michango kwa ajili ya wagonjwa wa kansa wa Hospitali ya  Ocean Road.

dk-kigwangalla-4
  …Akiendelea na hotuba. 

dk-kigwangalla-2

dk-kigwangalla-3

Baadhi ya watu waliojitokeza jana kwenye zoezi hilo.

NAIBU Waziri  wa Afya, Maendeleo ya Jamii,  Jinsia,  Wazee na Watoto  Dk. Hamisi Kigwangalla  jana aliongoza  matembezi  ya kukusanya michango kwa ajili ya  kusaidia wagonjwa wanaosumbuliwa na tatizo la kansa katika hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam.
  Waziri huyo alisema ili kuondokana na tatizo la kansa ni lazima tuwe na utaratibu wa  kupima afya zetu mapema kwani itasaidia kwa wale wenye dalili za mapema za ugonjwa huo kupona kabisa.
   “Saratani ya matiti na shingo ya kizazi ikigundulika mapema ikiwa katika hatua za awali mgonjwa anaweza kupona kabisa,” alisema Kingwangala.
  Pia alifafanua kuwa ni asilimia kumi tu ya wagonjwa wenye tatizo la kansa wanaofika hospitali mapema, badala yake wengi wao hufika hospitali hatua za mwisho wanapokuwa wamezidiwa.
   Aidha aliongeza kuwa    serikali imeanza mkakati  wa kuzuia na kudhibiti  saratani ambao umekwisha zinduliwa na kutoa chanjo kwa wasichana.
Kupata video ya tukio hili tembelea Youtube Chaneli yetu ya Global TV Online,  au katika website ya www.globaltvtz.com

Na Hilaly Daud/GPL