
Maziko ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Azam, Said Mohammed yakifanyika katika Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo.

Mwili wa Said Mohammed ukipelekwa makaburini kwa maziko.

Mwili wa Said Mohammed ukishushwa kwenye gari eneo la makaburini.

Rais wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodgar Chilla Tenga (wa pili kulia) akiwa makaburini.

Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi (wa pili kulia) naye alikuwepo.
MAMIA ya Watanzania leo wamejitokeza kumzika aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Azam, Said Mohammed aliyefariki dunia juzi Jumatatu.
Marehemu Said alikutwa na umauti katika Hospitali ya Agha Khan alikokuwa amelazwa kwa matibabu na amezikwa katika Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam baada ya swala ya alasiri.
Miongoni mwa waliohudhuria mazishi hayo ni pamoja na Rais wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodgar Chilla Tenga aliyeambatana na viongozi wengine wa TFF akiwemo Rais Jamal Malinzi pamoja na familia ya marehemu na wachezaji wa Klabu ya Azam Kikosi B.
Akiongea na tovuti hii, Tenga ambaye pia ni bosi ndani ya Shirikisho la Soka Afrika (Caf) alisema: “Ni msiba mkubwa na katu pengo lake haliwezi kuzibika. Mzee Said alifanya mambo mengi katika maendeleo ya soka letu na ndiyo maana bado alikuwa kiongozi wa mpira wetu mpaka anatutoka. Kuna kila sababu ya kuyaendeleza yale mazuri aliyotufanyia kwa tija ya maendeleo ya soka letu.”
Mpaka anafariki, Said Mohammed alikuwa pia ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi.
Habari / Picha: Sweetbert Lukonge na Wilbert Molandi / GPL





