×

Waziri Mkuu Awapongeza Watanzania Walioshiriki Kongamano La Uchumi Urusi

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Rais wa Urusi, Vladimir Putin wakati alipohudhuria gwaride la Jeshi la Wanamaji la nchi hiyo lililofanyika St. Petersburg nchini Urusi, Julai 30, 2023. Kushoto ni mkewe Mama Mary Majaliwa.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewapongeza wafanyabiashara 19 kutoka Tanzania ambao walishiriki maonesho ya kibiashara kwenye Jukwaa la Kimataifa la Uchumi na Kibinadamu la Afrika na Urusi lililomalizika Julai 28, mwaka huu.

Wafanyabiashara hao wanamiliki makampuni yanayohusika na sekta za elimu, afya, kilimo, madini, mafuta na gesi, utalii, ujenzi, utafiti na ushauri wa kibiashara.

Ametoa pongezi hizo jana jioni (Jumamosi, Julai 29, 2023) wakati akizungumza nao jijini St. Petersburg, Urusi ambako alimwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Mkutano wa Pili wa Kilele baina ya Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka mataifa ya Afrika na Urusi.

Leave a Comment