×

Miss Uganda Mwaka 1972 Afariki Dunia

charlotte-ssaliKAMPALA, UGANDA: Aliyewahi kuwa Miss Uganda, Charlotte Ssali, amefariki dunia leo asubuhi akiwa katika Hospitali ya Mulago alikokuwa akitibiwa.

Ripoti ya madaktari bado haijatoka kuhusiana na kifo cha staa huyo huku familia nayo ikiwa haijazungumza chochote kuhusu taratibu zamsiba huo.

Ssali, ambaye ni Miss Uganda wa mwaka 1972 ni mtoto wa aliyekuwa daktari maarufu wa Hospitali ya Mulago, Ssali ambaye kwa sasa ni marehemu.

Baada ya kukabidhi taji hilo kwa aliyemfuatia Charlotte alifanya kazi mbalimbali ikiwemo ya utangazaji katika televisheni ya UTV, na mpaka mauti yanamkuta alikuwa akitangaza katika televisheni ya UBC.

MWENYEZI MUNGU AMREHEMU CHARLOTTE SSALI, APUMZIKE KWA AMNI. AMINA