×

Mwijage Akaribisha Miradi Kutoka Nje

1

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, akizungumza na wafanyabiashara kutoka Ubelgiji.

2

Meza kuu ilivyoonekana.

3

Mwakilishi wa kundi la wafanyabiashara wa Umoja wa Ulaya (EU) Rose Blackie, akizungumza katika hafla hiyo.

4

Baadhi ya wafanyabiashara wakiwa katika hafla hiyo.

5

 Shughuli zikiendelea.

WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, amesema kuwa milango ya uwekezaji nchini ipo wazi hivyo wawekezaji kutoka nje ya nchi wamekaribishwa kuwekeza katika fursa nyingi zilizopo.

Ameyasema hayo leo katika mkutano wa wafanyabiashara wa Tanzania na Ubelgiji uliofanyika jijini Dar es Salaam amesema mazingira yaliyopo ni bora kwa uwekezaji wa biashara kupitia Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC).

“Tanzania ni nchi inayokua kwa kasi duniani hivyo wawekezaji wana nafasi ya kufanya uwekezaji kutokana na kwamba hii ni nchi ya amani ambapo wanaweza kuwekeza na kuzalisha bila kuwepo kwa vikwazo,” alisema Mwijage.

Aliongeza kwamba miongoni mwa mambo yanayoweza kuwekezwa ni kilimo, usafirishaji, uboreshaji wa miundombinu ambapo alisema Mkoa wa Kigoma unazo fursa nyingi ikiwemo kilimo cha michikichi na miwa kwa kuzalisha sukari.
Alisema Tanzania na Ubelgiji zimekuwa na ushirikiano wa muda mrefu, hivyo milango ya uwekezaji ipo wazi kwa kuwekeza katika mradi wowote.

Na Denis Mtima/Gpl