×

Wapwa wa Rais Watiwa Mbaroni kwa Kuingiza Kilo 800 za Cocaine, Marekani

venezueraMAREKANI: WAPWA wawili wa Rais wa Venezuela, Nicolás Maduro wamepatikana na hatia ya kujaribu kuingiza takribani Kilogramu 800 za Mihadarati aina ya Cocaine nchini Marekani.

Efrain Antonio Campo Flores, miaka 30, na Franqui Francisco Flores de Freitas, miaka 31, kila mmoja alikutwa na kosa la kupanga njama za kusafirisha madawa hayona sasa watatumikia kifungo gerezani.

Uchunguzi uliofanywa na Maafisa wa Marekani umebaini kuwa watuhumiwa walipanga kusafirisha madawa hayo kutoka Venezuela kisha Honduras hatimaye Marekani kwa kutumia ndege, wakitegemea kutengeneza mamilioni ya faida.

Katika upelelezi uliofanywa kwa muda wa chini ya wiki mbili wabainisha kuwa watuhumiwa waliwahi kukamatwa na Mamlaka ya Kuzuia Madawa ya kulevya ya Haiti mwaka jana.

Source: The Wall Street Journal

halotel-strip-1