Mshindi wa tuzo tatu za EATV 2016, Mwanamuziki Ali Kiba akiwadatisha mashabiki waliofurika katika ufukwe wa Escape One jana kushuhudia tamasha la After Skul Bash.
Weusi juu ya stage wakiongozwa na Joh Makini, Nikki wa Pili na G Nako.
Mkali wa ngoma inayohit kwa sasa iitwayo Muziki, Darassa akilishambulia jukwaa la After Skul Bash.
Prince Dully Sykes akisema na mashabiki wake.
Mwanamuziki Msami Baby na vijana wake wakiburudisha nyomi iliyotia timu katika tamasha hilo.
Mo Music akiwaimbisha mashabiki.
Mwanamuziki anayefanya vyema katika Muziki wa Singeli, Sholo Mwamba akikamua ngoma yake iitwayo Gheto.
Mwana Hip hop Izzo Bizness akiwa na mashabiki stejini.
Wanamuziki Ali Kiba na Ommy Dimpoz wakipafomu ngoma yao ya Kajiandae kwa pamoja stejini.
Ali Kiba na Ommy Dimpoz wakizidi kuwapa raha mashabiki wa muziki.
MC wa tamasha hilo, Perfect Clisspin (kushoto) akiwa na Miss and Mr After Skul Bash.
Mwana FA akifanya makamuzi katika tamasha hilo.
Dyna Nyange akifanya yake.
WANAVYUO mbalimbali jana walikutana pembezoni mwa Ufukwe wa Bahari ya Hindi, katika Kiwanja cha Escape One ambapo kulikuwa na full shangwe ya Tamasha la After Skul Bash.
Wanavyuo walioibuka kuwa Miss na Mr After Skul Bash walitangaziwa kupata ofa ya kushiriki chakula cha mchana na Msanii wa Bongo Fleva, Nassib Abdul na Miss Tanzania mwaka 2004, Faraja Kotta.
Wasanii waliosindikiza tamasha hilo ni Ali Kiba, Ommy Dimpoz, Fid Q, Mwana FA, Vee Money, Jux, Dully Sykes, Tammy, Msami, Barakah The Prince, Darasa, Weusi, Izzo Businez, Young D, Young Killer, Ned Music, Mo Music, Dayna Nyange, Chemical, Ay na wengine wengi.
Wapenzi wa burudani walifurika vya kutosha katika tamasha hilo lililoandaliwa na Clouds FM, Kupitia Kipindi cha XXL huku host wa tamasha hilo akiwa ni mtangazaji wa kituo hicho, Perfect Clisspin.
Video: After School Bash 2016
Video: After School Bash 2016, AY Alivyokinukisha



















