Ajibu Amrahisishia Kazi Kagere

IBRAHIM Ajibu, nyota wa Simba aliyejiunga msimu huu akitokea Yanga ameweka wazi kuwa amejipanga kutoa asisti zaidi ya 17 alizotoa akiwa Yanga msimu uliopita na mabao sita aliyofunga.

 

Mechi ya kwanza ya mashindano akiwa na Simba alicheza juzi, aliingia dakika ya 77 akichukua nafasi ya Clatous Chama katika mchezo dhidi ya JKT Tanzania, Simba ilishinda 3-1.

 

Ajibu alisema kuwa, kwa uwezo wa Mungu anaamini atafanya vyema na kuhusu asisti huenda
akazipiga zaidi ya msimu uliopita akiwa na Yanga hali ambayo inatafsiri kuwa washambuliaji wa Simba wakiongozwa na Meddie Kagere watafunga sana mabao kupitia pasi za Ajibu.

 

“Ndiyo kwanza ligi imeanza lakini kwa uwezo wa Mungu nina amini nitafanya vizuri na kuhusu zile asisti za msimu uliopita huenda nikatoa zaidi lakini kikubwa ni kujipanga na kushinda.

 

“Naomba mashabiki wa Simba waendelee tu kutusapoti kwa nguvu zote, mimi nawapenda wote kama ambavyo wao wananipenda na zawadi yao ni sisi kupambana kupata ushindi tu,” alisema Ajibu.


Loading...

Toa comment