The House of Favourite Newspapers

Ajibu: Kazi ndiyo imeanza

IBRAHIM Ajibu, kiungo mshambuliaji wa Simba amesema kuwa mashabiki wanapaswa waendelee kutoa sapoti ya kutosha kwani kazi ndiyo kwanza imeanza.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, hili, Ajibu alisema kuwa timu imeanza kwa kasi kutokana na ubora wa kikosi pamoja na ushirikiano uliopo jambo linalowapa nafasi ya kushinda michezo yao.

 

“Kila mechi kwetu ni muhimu na tunacheza kwa kuamini kwamba ushindani ni mkubwa ila bado tutaendelea kupambana.

 

“Kazi bado ipo kutokana na ukweli kwamba michezo ipo mingi kushinda kwetu michezo ya mwanzo kunatuongezea hali ya kujiamini katika michezo inayofuata,” alisema. Msimu uliopita akiwa Yanga alitoa asisti 17, lakini hadi sasa akiwa ndani ya Simba ametoa moja.

Comments are closed.