Albamu Harmo Tishio Boomplay

ALBAMU ya High School ya staa wa Bongo wa Fleva, Harmonize imefikisha zaidi ya Streams milioni 10 kwenye mtandao wa Boomplay ikiwa ni siku 28 tu tangu aiachie rasmi.

 

High School ni albamu ya pili ya Harmonize ambayo aliiachia November 5, 2021 ikiwa na jumla ya nyimbo 18.

 

Haya ni mafaniko makubwa kwa Harmonize ukilinganisha na albamu yake ya kwanza Afro East aliyoiachia Machi 14, 2020 ambayo mpaka sasa ina jumla ya streams milioni 2.6 kwenye mtandao huo wa Boomplay.


Toa comment