The House of Favourite Newspapers
gunners X

Aliyekua Mshauri wa Trump Ashtakiwa Kwa Kuvujisha Siri za Taifa

0

John Bolton, aliyekuwa mshauri wa usalama wa taifa wa Rais Donald Trump na kisha akawa mkosoaji wake makini, amefunguliwa mashtaka ya jinai ya shirikisho.

Hii inatokea baada ya maafisa wa FBI kukagua makazi na ofisi za Bolton Agosti katika uchunguzi kuhusu namna alivyoshughulikia taarifa za siri za kitaifa.

Kesi ya mashtaka yenye kurasa 26, iliyowasilishwa mahakamani Greenbelt, Maryland, Alhamisi, inamkashifu Bolton kwa makosa 8 ya kuhamisha taarifa za ulinzi wa taifa (NDI) na makosa 10 ya kushikilia NDI kinyume cha sheria.

Wakili wa mashtaka wanasema alihamisha kinyume cha sheria taarifa za siri kuhusu ulinzi wa taifa kupitia barua pepe za kibinafsi na programu nyingine za ujumbe.

Hati za mahakama zinasema, “Hati hizi zilifichua taarifa za kijasusi kuhusu mashambulio yajayo, adui wa kigeni, na uhusiano wa sera za kigeni.”

Ikiwa atapatikana na hatia, Bolton anaweza kufungwa hadi miaka 10 kwa kila kosa. Anatarajiwa kujisalimisha kwa mamlaka Alhameisi. “Hakuna anayeyekua juu ya sheria,” alisema Katibu Mkuu wa Sheria ya Marekani, Pam Bondi.

🔴Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV — usisahau ku-like, ku-comment na ku-subscribe ili uendelee kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.

Leave A Reply