The House of Favourite Newspapers

Amuua Mama Yake kwa Shoka, Anywa Damu Yake – Video

0

POLISI mkoani Arusha, linamshikilia Daniel Emmanuel (32) Mkazi wa Sakila wilayani Arumeru, kwa kukutwa akinywa damu ya mama yake mzazi Eliyamulika Emmanuel Sarakikiya (79) kwenye kikombe, baada ya kumuua kwa kumkata na shoka kisha kutenganisha shingo, mkono, mguu na kiwiliwili.

 

Wakati anafanya hivyo alikuwa anakinga damu kwenye kikombe anakunywa na Kamanda wa polisi Mkoani Arusha, Jonathan Shanna amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Baada ya tukio hilo mtuhumiwa alichukua kikombe cha maji na kukinga damu iliyokuwa ikichuruzika kwenye majeraha na kunywa jambo lililowastaajabisha wakazi wengi wa eneo hilo. Hata hivyo polisi waliofika eneo la tukio hawakukuta damu yoyote ya marehemu baada ya mtuhumiwa kufanikiwa kuinywa kwa lengo la kupoteza ushahidi.

 

Shanna amedai kuwa mtuhumiwa alijaribu kukimbia baada ya kuwaona polisi, hata hivyo askari hao walifanikiwa kumkamata na kwamba baada ya kufikishwa kituo cha polisi amegoma kuongea chochote.

 

Aidha, mtuhumiwa atafikishwa katika hospital ya Mkoa Mount meru kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi ili kubaini iwapo ana matatizo ya akili na atafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika. Shanna ametoa wito kwa jamii kuacha kuishi kwa mazoea na mtu anayedhaniwa kuwa na matatizo ya akili badala yake iwapeleke katika hospital kwa ajili ya uchunguzi zaidi na matibabu. 

 

Leave A Reply