The House of Favourite Newspapers

URAFIKI WA AUNT NA WEMA HATA KWA GREDA HAUVUNJIKI

Aunt Ezekiel na Wema Isaac Sepetu.

Mastaa wawili wa filamu Bongo Movies, Aunt Ezekiel na Wema Isaac Sepetu wamefunguka kuwa urafiki wao hata lije greda la ukubwa gani, bado litashindwa kuuvunja kwa sababu umejengwa kwa upendo mkubwa, jambo linalowafanya watu wengi washindwe kuwago-mbanisha.

 

Akizungumza na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Aunt alisema mara nyingi hata wakigombana na kila mmoja kuwa na mambo yake, bado inapotokea mmoja amepata tatizo, lazima mwingine atasimama kwa ajili ya mwenzake bila kujali tofauti zao.

 

“Unajua urafiki mzuri siyo wakati mkiwa katika kipindi cha furaha tu, bali ni lazima kusimama kotekote, yaani kwenye raha na shida, siyo kwamba hatugombani, tunagombana ila kila mmoja anatambua thamani ya mwenzake,” alisema Aunt.

 

Kwa upande wa Wema, alisema Aunt ‘amekava’ kila kitu kwake kwani ndiye rafiki wa kweli kwenye maisha yake ya kila siku na hata wanapogombana ni kama wanachaji urafiki wao uzidi kukolea siku hadi siku.

 

“Aunt ni rafiki ninayemuhitaji kwenye maisha yangu yaani anafunika kila kitu kwa sababu kwenye shida zangu kubwa na ndogo yupo, sasa hapo ni nani ambaye anaweza kuuvunja urafiki wetu? Naamini hakuna,” alisema Wema.

STORI NA IMELDA MTEMA 

VITUKO Vya RC MWANRI Stejini Wasafi Festival “SUKUMA NDANI”

Comments are closed.