The House of Favourite Newspapers

Aunt, Kusah vs Ruby Kimeumana!

0

MAMBO yanazidi kuharibika baina ya mastaa watatu ambao mapenzi yamewatoa uvumilivu na kuwa kwenye vute nikuvute kisha kuanikana hadharani na sasa vita inazidi kuwa kali zaidi.

 

Sakata hilo linamhusisha staa mkubwa wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel na mzazi mwenzake, Salmin Hoza au Kusah ambao wanapambana dhidi ya staa wa Bongo Fleva, Hellen George au Ruby.


Aunt na Ruby; kwa pamoja
wamebarikiwa kupata mtoto na Kusah, lakini inaonekana kuwa penzi la jamaa huyo
linawasumbua kinoma.

 

Awali, chokochoko zilianza baada ya Ruby kuibuka kuwa anatoka kimapenzi na mzazi mwenza wa Aunty ambaye ni Moze Iyobo.

 

Hapo ndipo vita iliponoga, lakini kwa upande wa Aunt na Kusah wakawa kama hawaioni drama inayoendelea, lakini sasa sakata limegeukia kwenye malezi ya mtoto wa Ruby wa kike aliyezaa na Kusah.

 

Akiwa jukwaani kwenye tamasha la wasanii lililofanyika Bagamoyo wiki iliyopita, Ruby alitupa madongo kwa Aunt na Kusah na hata kusema kuwa hahitaji takataka, lakini mapokeo ya upande wa pili yakawa tofauti kwani ndiyo kwanza wakatangaza ndoa na picha kusambaa siku ambayo ilikuwa kumbukizi ya siku ya kuzaliwa ya Aunt.


Sakata hilo; hivi sasa
limechukua sura mpya baada ya Ruby kusema kuwa, Kusah hamjali mtoto wala kumuhudumia kwa chochote.
Lakini wakati huohuo, Kusah anadai kuwa, Ruby siyo mlezi bora wa mtoto hivyo asitafute mchawi.


“Yaani ukweli ni kwamba Ruby
aache mambo ya kusingizia vitu ambavyo havipo, anachotakiwa kufanya ni kumjali mwanawe maana hakuwa anafanya hivyo na sijui kwa nini,” anasema Kusah.


Kwa upande wake, Aunt
anasema kuwa, hana tatizo lolote na siku mtoto wa Kusah na Ruby akiletwa kwake atampokea vizuri kwa sababu ni dada wa mwanawe aitwaye Nono aliyezaa na Kusah.

Leave A Reply