×

Aweso Atinga Dawasa Usiku.. Atoa Maagizo Mazito Kwa Menejimenti

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso (Mb) usiku wa kuamkia leo Novemba 18, 2021 ametinga kwenye Ofisi za DAWASA kuwekea msisitizo mambo mbalimbali kwenye kipindi hiki ambacho Dar es salaam imekumbwa na mgao wa maji ambapo mojawapo ya aliyoyasisitiza ni mgao wa maji kutolewa kwa uwiano na bila upendeleo.

Kwenye kikao hicho kirefu cha mikakati kilichofanyika usiku, Waziri aliongoza majadiliano ya suluhu ya muda mfupi na muda mrefu ya tatizo hili la maji pamoja na kuwapa hamasa Watumishi katika kipindi hiki kigumu na kuwataka Wataalamu watumie ubunifu na maarifa yao yote usiku na mchana kuwasaidia Wakazi wa Dar es salaam.

Jambo jingine muhimu alilolisisitiza Waziri Aweso ni kuitaka DAWASA kutoa bei elekezi kwa watoa huduma binafsi wa maji kupitia magari (bowsers) na kumalizia kwa ahadi ya ushirikiano wa Wizara katika kukabiliana na changamoto zilizopo kwa DAWASA na Bonde la Wami Ruvu.

#LIVE: MOSHI MWEUPE BANDARI YA BAGAMOYO, KUHAMIA LINDI |DIARY YA MBOWE YAZUA JAMBO | FRONT PAGE….

Leave a Comment