Azam FC: Tupo tayari kukichafua Ligi kuu

Image result for uongozi wa timu ya Azam FC

UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa timu yao ipo tayari kwa ajili ya msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu,Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’, alisema kikosi chao kipo tayari kupambana kwenye Ligi Kuu Bara msimu huu hususan kuelekea kwenye mchezo wao wa kwanza dhidi ya KMC kesho Jumanne huku akiwaomba mashabiki waendelee kuiunga mkono timu hiyo.

 

“Kikosi kipo tayari kwa msimu huu mpya hususan kwenye mchezo wetu wa kwanza dhidi ya KMC siku ya Jumanne, lakini nichukue nafasi hii kuwaomba mashabiki waendelee kuiunga mkono timu yetu kama walivyofanya kwenye mchezo wetu dhidi ya Fasil Kenema,” alisema Popat.


Loading...

Toa comment